Zaburi 70:3
Psalms 70:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Wale waniambiao, “Aha! Aha!” warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao.
Psalms 70:3 in English
Psalms 70:3 · Berean Standard Bible
May those who say, “Aha, aha!” retreat because of their shame.
Context
1Ee Mungu, ufanye haraka kuniokoa;
Ee Bwana, njoo hima unisaidie. 2Wale wanaotafuta kuuondoa uhai wangu,
waaibishwe na kufadhaishwa;
wote wanaotamani kuangamizwa kwangu,
warudishwe nyuma kwa aibu. 3Wale waniambiao, “Aha! Aha!”
warudi nyuma kwa sababu ya aibu yao. 4Lakini wote wakutafutao
washangilie na kukufurahia,
wale wapendao wokovu wako siku zote waseme,
“Mungu na atukuzwe!” 5Lakini bado mimi ni maskini na mhitaji;
Ee Mungu, unijie haraka.
Wewe ndiwe msaada wangu na mwokozi wangu;
Ee Bwana, usikawie.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.