Native Bible

Psalms 69:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu.

Psalms 69:15 in English

Psalms 69:15 · Berean Standard Bible

Do not let the floods engulf me or the depths swallow me up; let not the Pit close its mouth over me.

Context

13Lakini Ee Bwana, ninakuomba, kwa wakati ukupendezao; katika upendo wako mkuu, Ee Mungu, unijibu kwa wokovu wako wa hakika. 14Uniokoe katika matope, usiniache nizame; niokoe na hao wanichukiao, kutoka kwenye vilindi vya maji. 15Usiache mafuriko yanigharikishe au vilindi vinimeze, au shimo lifumbe kinywa chake juu yangu. 16Ee Bwana, unijibu, kwa wema wa upendo wako; kwa huruma zako nyingi unigeukie. 17Usimfiche mtumishi wako uso wako, uharakishe kunijibu, kwa sababu niko katika shida.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.