Zaburi 68:26
Psalms 68:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa, msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli.
Psalms 68:26 in English
Psalms 68:26 · Berean Standard Bible
Bless God in the great congregation; bless the LORD from the fountain of Israel.
Context
24Ee Mungu, maandamano yako yameonekana,
maandamano ya Mungu wangu, Mfalme wangu,
yakielekea patakatifu pake. 25Mbele wako waimbaji, baada yao wapiga vinanda,
pamoja nao wako wanawali wakipiga matari. 26Msifuni Mungu katika kusanyiko kubwa,
msifuni Bwana katika kusanyiko la Israeli. 27Liko kabila dogo la Benyamini likiwaongoza,
wakifuatwa na kundi kubwa la watawala wa Yuda,
hatimaye watawala wa Zabuloni na Naftali. 28Ee Mungu, amuru uwezo wako,
Ee Mungu tuonyeshe nguvu zako,
kama ulivyofanya hapo awali.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.