Native Bible

Psalms 64:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?”

Psalms 64:5 in English

Psalms 64:5 · Berean Standard Bible

They hold fast to their evil purpose; they speak of hiding their snares. “Who will see them?” they say.

Context

3Wananoa ndimi zao kama panga na kuelekeza maneno yao kama mishale ya kufisha. 4Hurusha mishale kutoka kwenye mavizio kwa mtu asiye na hatia, humrushia ghafula bila woga. 5Kila mmoja humtia moyo mwenzake katika mipango mibaya; huzungumza juu ya kuficha mitego yao, nao husema, “Ni nani ataiona?” 6Hufanya shauri baya la dhuluma na kusema, “Tumebuni mpango mkamilifu!” Hakika nia na moyo wa mwanadamu vina hila. 7Bali Mungu atawapiga kwa mishale, nao ghafula wataangushwa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.