Zaburi 63:3
Psalms 63:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai, midomo yangu itakuadhimisha.
Psalms 63:3 in English
Psalms 63:3 · Berean Standard Bible
Because Your loving devotion is better than life, my lips will glorify You.
Context
1Ee Mungu, wewe ni Mungu wangu,
nakutafuta kwa moyo wote;
nafsi yangu inakuonea kiu,
mwili wangu unakuonea wewe shauku,
katika nchi kame na iliyochoka
mahali ambapo hapana maji. 2Nimekuona katika mahali patakatifu
na kuuona uwezo wako na utukufu wako. 3Kwa sababu upendo wako ni bora kuliko uhai,
midomo yangu itakuadhimisha. 4Nitakusifu siku zote za maisha yangu,
na kwa jina lako nitainua mikono yangu. 5Nafsi yangu itatoshelezwa
kama kwa wingi wa vyakula;
kwa midomo iimbayo
kinywa changu kitakusifu wewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.