Zaburi 62:5
Psalms 62:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake, tumaini langu latoka kwake.
Psalms 62:5 in English
Psalms 62:5 · Berean Standard Bible
Rest in God alone, O my soul, for my hope comes from Him.
Context
3Mtamshambulia mtu hata lini?
Je, ninyi nyote mtamtupa chini,
ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? 4Walikusudia kikamilifu kumwangusha
toka mahali pake pa fahari;
wanafurahia uongo.
Kwa vinywa vyao hubariki,
lakini ndani ya mioyo yao hulaani. 5Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,
tumaini langu latoka kwake. 6Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
ndiye ngome yangu, sitatikisika. 7Wokovu wangu na heshima yangu viko kwa Mungu,
ndiye mwamba wangu wenye nguvu
na kimbilio langu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.