Zaburi 62:3
Psalms 62:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika?
Psalms 62:3 in English
Psalms 62:3 · Berean Standard Bible
How long will you threaten a man? Will all of you throw him down like a leaning wall or a tottering fence?
Context
1Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko;
wokovu wangu watoka kwake. 2Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu;
yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. 3Mtamshambulia mtu hata lini?
Je, ninyi nyote mtamtupa chini,
ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? 4Walikusudia kikamilifu kumwangusha
toka mahali pake pa fahari;
wanafurahia uongo.
Kwa vinywa vyao hubariki,
lakini ndani ya mioyo yao hulaani. 5Ee nafsi yangu, upumzike, kwa Mungu peke yake,
tumaini langu latoka kwake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.