Native Bible

Psalms 62:2 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe.

Psalms 62:2 in English

Psalms 62:2 · Berean Standard Bible

He alone is my rock and my salvation. He is my fortress; I will never be shaken.

Context

1Kwa Mungu peke yake nafsi yangu inapata pumziko; wokovu wangu watoka kwake. 2Yeye peke yake ndiye mwamba wangu na wokovu wangu; yeye ni ngome yangu, sitatikisika kamwe. 3Mtamshambulia mtu hata lini? Je, ninyi nyote mtamtupa chini, ukuta huu ulioinama na uzio huu unaotikisika? 4Walikusudia kikamilifu kumwangusha toka mahali pake pa fahari; wanafurahia uongo. Kwa vinywa vyao hubariki, lakini ndani ya mioyo yao hulaani.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.