Native Bible

Psalms 57:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko.

Psalms 57:8 in English

Psalms 57:8 · Berean Standard Bible

Awake, my glory!* Awake, O harp and lyre! I will awaken the dawn.

Context

6Waliitegea miguu yangu nyavu, nikainamishwa chini na dhiki. Wamechimba shimo katika njia yangu, lakini wametumbukia humo wao wenyewe. 7Ee Mungu, moyo wangu ni thabiti; nitaimba na kusifu kwa moyo wangu wote. 8Amka, nafsi yangu! Amka, kinubi na zeze! Nitayaamsha mapambazuko. 9Nitakusifu wewe, Ee Bwana, katikati ya mataifa; nitaimba habari zako, katikati ya jamaa za watu. 10Kwa maana upendo wako ni mkuu, waenea hadi mbinguni, uaminifu wako unazifikia anga.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.