Native Bible

Psalms 49:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao.

Psalms 49:10 in English

Psalms 49:10 · Berean Standard Bible

For it is clear that wise men die, and the foolish and the senseless both perish and leave their wealth to others.

Context

8Fidia ya uhai ni gharama kubwa, hakuna malipo yoyote yanayotosha, 9ili kwamba aishi milele na asione uharibifu. 10Wote wanaona kwamba watu wenye hekima hufa; wajinga na wapumbavu vivyo hivyo huangamia na kuwaachia wengine mali zao. 11Makaburi yao yatabaki kuwa nyumba zao za milele, makao yao vizazi vyote; ingawa walikuwa na mashamba na kuyaita kwa majina yao. 12Lakini mwanadamu, licha ya utajiri wake, hadumu; anafanana na mnyama aangamiaye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.