Zaburi 39:11
Psalms 39:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Unakemea na kuadhibu wanadamu kwa ajili ya dhambi zao; unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo: kila mwanadamu ni kama pumzi tu.
Psalms 39:11 in English
Psalms 39:11 · Berean Standard Bible
You discipline and correct a man for his iniquity, consuming like a moth what he holds dear; surely each man is but a vapor. Selah
Context
9Nilinyamaza kimya,
sikufumbua kinywa changu,
kwa sababu wewe ndiwe uliyetenda hili. 10Niondolee mjeledi wako,
nimeshindwa kwa mapigo ya mkono wako. 11Unakemea na kuadhibu wanadamu
kwa ajili ya dhambi zao;
unaharibu utajiri wao kama nondo aharibuvyo:
kila mwanadamu ni kama pumzi tu. 12“Ee Bwana, usikie maombi yangu,
usikie kilio changu unisaidie,
usiwe kiziwi kwa kulia kwangu.
Kwani mimi ninaishi na wewe kama mgeni,
kama walivyokuwa baba zangu wote, 13Tazama mbali nami, ili niweze kufurahi tena
kabla sijaondoka na nisiwepo tena.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.