Native Bible

Psalms 36:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako.

Psalms 36:7 in English

Psalms 36:7 · Berean Standard Bible

How precious is Your loving devotion, O God, that the children of men take refuge in the shadow of Your wings!

Context

5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni, uaminifu wako hadi kwenye anga. 6Haki yako ni kama milima mikubwa, hukumu zako ni kama kilindi kikuu. Ee Bwana, wewe huwahifadhi mwanadamu na mnyama. 7Upendo wako usiokoma ni wa thamani mno! Watu wakuu na wadogo hujificha uvulini wa mbawa zako. 8Wanajifurahisha katika wingi nyumbani mwako, nawe utawanywesha katika mto wa furaha zako. 9Kuwa pamoja nawe ni kijito cha uzima, katika nuru yako twaona nuru.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.