Zaburi 36:4
Psalms 36:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya, hujitia katika njia ya dhambi na hakatai lililo baya.
Psalms 36:4 in English
Psalms 36:4 · Berean Standard Bible
Even on his bed he plots wickedness; he sets himself on a path that is not good; he fails to reject evil.
Context
2Kwa kuwa machoni pake mwenyewe hujisifu mno
hata hawezi kugundua au kuichukia dhambi yake. 3Maneno ya kinywa chake ni maovu na ya udanganyifu,
ameacha kuwa mwenye hekima na kutenda mema. 4Hata kitandani mwake hupanga hila mbaya,
hujitia katika njia ya dhambi
na hakatai lililo baya. 5Upendo wako, Ee Bwana, unafika hadi mbinguni,
uaminifu wako hadi kwenye anga. 6Haki yako ni kama milima mikubwa,
hukumu zako ni kama kilindi kikuu.
Ee Bwana, wewe huwahifadhi
mwanadamu na mnyama.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.