Zaburi 35:9
Psalms 35:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana na kuufurahia wokovu wake.
Psalms 35:9 in English
Psalms 35:9 · Berean Standard Bible
Then my soul will rejoice in the LORD and exult in His salvation.
Context
7Kwa vile walinifichia wavu wao bila sababu,
na bila sababu wamenichimbia shimo, 8maafa na yawapate ghafula:
wavu walionifichia na uwatege wenyewe,
na waanguke katika shimo hilo,
kwa maangamizo yao. 9Ndipo nafsi yangu itashangilia katika Bwana
na kuufurahia wokovu wake. 10Nitapaza sauti yangu nikisema,
“Ni nani aliye kama wewe, Ee Bwana?
Wewe huwaokoa maskini kutokana na wale walio na nguvu kuliko wao,
maskini na mhitaji kutokana na wanaowanyangʼanya!” 11Mashahidi wakatili wanainuka,
wananiuliza mambo nisiyoyajua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.