Zaburi 28:6
Psalms 28:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana asifiwe, kwa maana amesikia kilio changu nikimwomba anihurumie.
Psalms 28:6 in English
Psalms 28:6 · Berean Standard Bible
Blessed be the LORD, for He has heard my cry for mercy.
Context
4Walipe sawasawa na matendo yao,
sawasawa na matendo yao maovu;
walipe sawasawa na kazi za mikono yao,
uwalipe wanavyostahili. 5Kwa kuwa hawaheshimu kazi za Bwana,
na yale ambayo mikono yake imetenda,
atawabomoa na kamwe
hatawajenga tena. 6Bwana asifiwe,
kwa maana amesikia kilio changu
nikimwomba anihurumie. 7Bwana ni nguvu zangu na ngao yangu,
moyo wangu umemtumaini yeye,
nami nimesaidiwa.
Moyo wangu unarukaruka kwa furaha
nami nitamshukuru kwa wimbo. 8Bwana ni nguvu ya watu wake,
ngome ya wokovu kwa mpakwa mafuta wake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.