Zaburi 27:7
Psalms 27:7 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana, unihurumie na unijibu.
Psalms 27:7 in English
Psalms 27:7 · Berean Standard Bible
Hear, O LORD, my voice when I call; be merciful and answer me.
Context
5Kwa kuwa siku ya shida,
atanihifadhi salama katika maskani yake,
atanificha uvulini mwa hema yake
na kuniweka juu kwenye mwamba. 6Kisha kichwa changu kitainuliwa
juu ya adui zangu wanaonizunguka.
Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe;
nitamwimbia Bwana na kumsifu. 7Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Bwana,
unihurumie na unijibu. 8Moyo wangu unasema kuhusu wewe,
“Utafute uso wake!”
Uso wako, Bwana “Nitautafuta.” 9Usinifiche uso wako,
usimkatae mtumishi wako kwa hasira;
wewe umekuwa msaada wangu.
Usinikatae wala usiniache,
Ee Mungu Mwokozi wangu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.