Zaburi 22:13
Psalms 22:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Simba wangurumao wanaorarua mawindo yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu.
Psalms 22:13 in English
Psalms 22:13 · Berean Standard Bible
They open their jaws against me like lions that roar and maul.
Context
11Usiwe mbali nami,
kwa maana shida iko karibu
na hakuna wa kunisaidia. 12Mafahali wengi wamenizunguka,
mafahali wa Bashani wenye nguvu
wamenizingira. 13Simba wangurumao wanaorarua mawindo
yao hupanua vinywa vyao dhidi yangu. 14Nimemiminwa kama maji,
mifupa yangu yote imetoka katika viungo vyake.
Moyo wangu umegeuka kuwa nta,
umeyeyuka ndani yangu. 15Nguvu zangu zimekauka kama kigae,
ulimi wangu umegandamana
na kaakaa la kinywa changu,
kwa sababu umenilaza
katika mavumbi ya kifo.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.