Native Bible

Psalms 138:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari.

Psalms 138:3 in English

Psalms 138:3 · Berean Standard Bible

On the day I called, You answered me; You emboldened me and strengthened my soul.*

Context

1Nitakusifu wewe, Ee Bwana, kwa moyo wangu wote, mbele ya “miungu” nitaimba sifa zako. 2Nitasujudu nikielekea Hekalu lako takatifu, nami nitalisifu jina lako kwa ajili ya upendo wako na uaminifu, kwa kuwa umelikuza jina lako na neno lako juu ya vitu vyote. 3Nilipoita, ulinijibu; ulinifanya jasiri na mwenye moyo hodari. 4Wafalme wote wa dunia wakusifu wewe Ee Bwana, wakati wanaposikia maneno ya kinywa chako. 5Wao na waimbe kuhusu njia za Bwana, kwa maana utukufu wa Bwana ni mkuu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.