Native Bible

Psalms 13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Listen to Zaburi 13
1Mpaka lini, Ee Bwana? Je, utanisahau milele? Utanificha uso wako mpaka lini? 2Nitapambana na mawazo yangu mpaka lini, na kila siku kuwa na majonzi moyoni mwangu? Adui zangu watanishinda mpaka lini? 3Nitazame, unijibu, Ee Bwana Mungu wangu. Yatie nuru macho yangu, ama sivyo nitalala usingizi wa mauti. 4Adui yangu atasema, “Nimemshinda,” nao adui zangu watashangilia nitakapoanguka. 5Lakini ninategemea upendo wako usiokoma; moyo wangu unashangilia katika wokovu wako. 6Nitamwimbia Bwana, kwa kuwa amekuwa mwema kwangu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.