Native Bible

Psalms 116:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni.

Psalms 116:3 in English

Psalms 116:3 · Berean Standard Bible

The ropes of death entangled me; the anguish of Sheol overcame me; I was confronted by trouble and sorrow.

Context

1Ninampenda Bwana kwa maana amesikia sauti yangu; amesikia kilio changu ili anihurumie. 2Kwa sababu amenitegea sikio lake, nitamwita siku zote za maisha yangu. 3Kamba za mauti zilinizunguka, maumivu makuu ya kuzimu yalinipata, nikalemewa na taabu na huzuni. 4Ndipo nikaliitia jina la Bwana: “Ee Bwana, niokoe!” 5Bwana ni mwenye neema na haki, Mungu wetu ni mwingi wa huruma.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.