Zaburi 115:3
Psalms 115:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mungu wetu yuko mbinguni, naye hufanya lolote limpendezalo.
Psalms 115:3 in English
Psalms 115:3 · Berean Standard Bible
Our God is in heaven; He does as He pleases.
Context
1Sio kwetu sisi, Ee Bwana, sio kwetu sisi,
bali utukufu ni kwa jina lako,
kwa sababu ya upendo
na uaminifu wako. 2Kwa nini mataifa waseme,
“Yuko wapi Mungu wao?” 3Mungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo. 4Lakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu. 5Zina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.