Zaburi 109:17
Psalms 109:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.
Psalms 109:17 in English
Psalms 109:17 · Berean Standard Bible
The cursing that he loved, may it fall on him; the blessing in which he refused to delight, may it be far from him.
Context
15Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana,
ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. 16Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema,
bali alimfukuza mnyonge na mhitaji,
aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. 17Alipenda kulaani,
nayo laana ikampata;
hakupenda kubariki,
kwa hiyo baraka na ikae mbali naye. 18Alivaa kulaani kama vazi lake,
nayo laana ikamwingia mwilini mwake kama maji,
kwenye mifupa yake kama mafuta. 19Na iwe kama joho alilozungushiwa,
kama mshipi aliofungiwa daima.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.