Native Bible

Psalms 109:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani.

Psalms 109:15 in English

Psalms 109:15 · Berean Standard Bible

May their sins always remain before the LORD, that He may cut off their memory from the earth.

Context

13Uzao wake na ukatiliwe mbali, majina yao yafutike katika kizazi kifuatacho. 14Maovu ya baba zake na yakumbukwe mbele za Bwana, dhambi ya mama yake isifutwe kamwe. 15Dhambi zao na zibaki daima mbele za Bwana, ili apate kukatilia mbali kumbukumbu lao duniani. 16Kwa maana kamwe hakuweza kutenda wema, bali alimfukuza mnyonge na mhitaji, aliwafanyia jeuri wahitaji na waliovunjika moyo. 17Alipenda kulaani, nayo laana ikampata; hakupenda kubariki, kwa hiyo baraka na ikae mbali naye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.