Native Bible

Psalms 106:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana.

Psalms 106:16 in English

Psalms 106:16 · Berean Standard Bible

In the camp they envied Moses, as well as Aaron, the holy one of the LORD.

Context

14Jangwani walitawaliwa na tamaa zao, walimjaribu Mungu nyikani. 15Kwa hiyo aliwapa kile walichoomba, lakini akatuma juu yao ugonjwa wa kudhoofisha. 16Kambini walimwonea wivu Mose, na pia Aroni aliyekuwa amewekwa wakfu kwa Bwana. 17Ardhi ilifunguka ikawameza Dathani, ikawazika Abiramu na kundi lake. 18Moto uliwaka katikati ya wafuasi wao, mwali wa moto uliwateketeza waovu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.