Native Bible

Psalms 102:23 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, akafupisha siku zangu.

Psalms 102:23 in English

Psalms 102:23 · Berean Standard Bible

He has broken my strength on the way; He has cut short my days.

Context

21Kwa hiyo jina la Bwana latangazwa huko Sayuni na sifa zake katika Yerusalemu, 22wakati mataifa na falme zitakapokusanyika ili kumwabudu Bwana. 23Katika kuishi kwangu alivunja nguvu zangu, akafupisha siku zangu. 24Ndipo niliposema: “Ee Mungu wangu, usinichukue katikati ya siku zangu; miaka yako inaendelea vizazi vyote. 25Hapo mwanzo uliweka misingi ya dunia, nazo mbingu ni kazi ya mikono yako.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.