Zaburi 101:4
Psalms 101:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami; nitajitenga na kila ubaya.
Psalms 101:4 in English
Psalms 101:4 · Berean Standard Bible
A perverse heart shall depart from me; I will know nothing of evil.
Context
2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:
utakuja kwangu lini?
Nitatembea nyumbani mwangu
kwa moyo usio na lawama. 3Sitaweka mbele ya macho yangu
kitu kiovu.
Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;
hawatashikamana nami. 4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;
nitajitenga na kila ubaya. 5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,
huyo nitamnyamazisha;
mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi
huyo sitamvumilia. 6Macho yangu yatawaelekea waaminifu katika nchi,
ili waweze kuishi pamoja nami;
yeye ambaye moyo wake hauna lawama
atanitumikia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.