Zaburi 101:3
Psalms 101:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Sitaweka mbele ya macho yangu kitu kiovu. Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani; hawatashikamana nami.
Psalms 101:3 in English
Psalms 101:3 · Berean Standard Bible
I will set no worthless thing before my eyes. I hate the work of those who fall away; it shall not cling to me.
Context
1Nitaimba juu ya upendo wako na haki yako;
kwako wewe, Ee Bwana, nitaimba sifa. 2Nitazingatia kuishi maisha yasiyo na lawama:
utakuja kwangu lini?
Nitatembea nyumbani mwangu
kwa moyo usio na lawama. 3Sitaweka mbele ya macho yangu
kitu kiovu.
Ninayachukia matendo ya watu wasio na imani;
hawatashikamana nami. 4Moyo wa ukaidi utakuwa mbali nami;
nitajitenga na kila ubaya. 5Kila amsingiziaye jirani yake kwa siri,
huyo nitamnyamazisha;
mwenye macho ya dharau na moyo wa kiburi
huyo sitamvumilia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.