Native Bible

Proverbs 30:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi.

Proverbs 30:25 in English

Proverbs 30:25 · Berean Standard Bible

The ants are creatures of little strength, yet they store up their food in the summer;

Context

23mwanamke asiyependwa aolewapo, naye mtumishi wa kike achukuapo nafasi ya bibi yake. 24“Vitu vinne duniani vilivyo vidogo, lakini vina akili nyingi sana: 25Mchwa ni viumbe wenye nguvu ndogo, hata hivyo hujiwekea akiba ya chakula chao wakati wa kiangazi. 26Pelele ni viumbe vyenye uwezo mdogo hata hivyo hujitengenezea nyumba zao kwenye miamba. 27Nzige hawana mfalme, hata hivyo huenda pamoja vikosi vikosi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.