Mithali 29:13
Proverbs 29:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili: Bwana hutia nuru macho yao wote wawili.
Proverbs 29:13 in English
Proverbs 29:13 · Berean Standard Bible
The poor man and the oppressor have this in common: The LORD gives light to the eyes of both.
Context
11Mpumbavu huonyesha hasira yake yote,
bali mwenye hekima hujizuia. 12Kama mtawala akisikiliza uongo,
maafisa wake wote huwa waovu. 13Mtu maskini na mtu anayeonea wanafanana kwa jambo hili:
Bwana hutia nuru macho yao wote wawili. 14Kama mfalme akiwaamua maskini kwa haki,
kiti chake cha enzi kitakuwa thabiti siku zote. 15Fimbo ya maonyo hutia hekima,
bali mtoto aliyeachiwa bila maonyo
humwaibisha mama yake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.