Mithali 26:25
Proverbs 26:25 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini, kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake.
Proverbs 26:25 in English
Proverbs 26:25 · Berean Standard Bible
When he speaks graciously, do not believe him, for seven abominations fill his heart.
Context
23Kama rangi ingʼaayo iliyopakwa kwenye vyombo vya udongo
ndivyo ilivyo midomo laini pamoja na moyo mbaya. 24Mtu mwenye nia ya kudhuru wengine hujificha kwa maneno ya midomo yake,
lakini moyoni mwake huficha udanganyifu. 25Ingawa maneno yake huvutia, usimwamini,
kwa maana machukizo saba hujaza moyo wake. 26Nia yake ya kudhuru wengine inaweza kufichwa na udanganyifu,
lakini uovu wake utafichuliwa kwenye kusanyiko. 27Kama mtu akichimba shimo, atatumbukia ndani yake,
kama mtu akivingirisha jiwe, litamrudia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.