Mithali 24:11
Proverbs 24:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo; wazuie wote wanaojikokota kuelekea machinjoni.
Proverbs 24:11 in English
Proverbs 24:11 · Berean Standard Bible
Rescue those being led away to death, and restrain those stumbling toward the slaughter.
Context
9Mipango ya upumbavu ni dhambi,
watu huchukizwa na mwenye dhihaka. 10Ukikata tamaa wakati wa taabu,
jinsi gani nguvu zako ni kidogo! 11Okoa wale wanaoongozwa kwenye kifo;
wazuie wote wanaojikokota
kuelekea machinjoni. 12Kama mkisema, “Lakini hatukujua lolote kuhusu hili,”
je, yule apimaye mioyo halitambui hili?
Je, yule awalindaye maisha yenu halijui hili?
Je, hatamlipa kila mtu kulingana na aliyotenda? 13Ule asali mwanangu, kwa kuwa ni nzuri;
asali kutoka kwenye sega ni tamu kwa kuonja.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.