Mithali 21:16
Proverbs 21:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu, hupumzika katika kundi la waliokufa.
Proverbs 21:16 in English
Proverbs 21:16 · Berean Standard Bible
The man who strays from the path of understanding will rest in the assembly of the dead.
Context
14Zawadi itolewayo kwa siri hutuliza hasira
na rushwa iliyofichwa kwenye nguo hutuliza ghadhabu kali. 15Wakati haki imetendeka, huleta furaha kwa wenye haki,
bali kitisho kwa watenda mabaya. 16Mtu anayepotea kutoka mapito ya ufahamu,
hupumzika katika kundi la waliokufa. 17Mtu apendaye anasa atakuwa maskini,
yeyote apendaye mvinyo na mafuta kamwe hatakuwa tajiri. 18Waovu huwa fidia kwa ajili ya wenye haki,
nao wasio waaminifu kwa ajili ya wanyofu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.