Mithali 21:10
Proverbs 21:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu mwovu hutamani sana ubaya, jirani yake hapati huruma kutoka kwake.
Proverbs 21:10 in English
Proverbs 21:10 · Berean Standard Bible
The soul of the wicked man craves evil; his neighbor finds no favor in his eyes.
Context
8Njia ya mwenye hatia ni ya upotovu,
bali tabia ya mtu asiye na hatia ni nyofu. 9Ni afadhali kuishi pembeni mwa paa la nyumba,
kuliko kuishi nyumba moja na mke mgomvi. 10Mtu mwovu hutamani sana ubaya,
jirani yake hapati huruma kutoka kwake. 11Wakati mwenye mzaha ameadhibiwa,
mjinga hupata hekima;
wakati mtu mwenye hekima afundishwapo,
hupata maarifa. 12Mwenye Haki huyajua yanayotendeka katika nyumba za waovu,
naye atawaangamiza waovu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.