Mithali 19:22
Proverbs 19:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho, afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo.
Proverbs 19:22 in English
Proverbs 19:22 · Berean Standard Bible
The desire of a man is loving devotion; better to be poor than a liar.
Context
20Sikiliza mashauri na ukubali mafundisho,
nawe mwishoni utakuwa na hekima. 21Kuna mipango mingi ndani ya moyo wa mtu,
lakini kusudi la Bwana ndilo litakalosimama. 22Lile mtu alionealo shauku ni upendo usio na mwisho,
afadhali kuwa maskini kuliko kuwa mwongo. 23Kumcha Bwana huongoza kwenye uzima,
kisha mtu hupumzika akiwa ameridhika,
bila kuguswa na shida. 24Mtu mvivu hutumbukiza mkono wake kwenye sahani,
lakini hawezi hata kuupeleka kwenye kinywa chake!
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.