Native Bible

Proverbs 19:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana.

Proverbs 19:14 in English

Proverbs 19:14 · Berean Standard Bible

Houses and wealth are inherited from fathers, but a prudent wife is from the LORD.

Context

12Ghadhabu ya mfalme ni kama mngurumo wa simba, bali wema wake ni kama umande juu ya nyasi. 13Mwana mpumbavu ni maangamizi ya babaye, naye mke mgomvi ni kama kutonatona kusikoisha. 14Nyumba na mali hurithiwa kutoka kwa wazazi, bali mke mwenye busara hutoka kwa Bwana. 15Uvivu huleta usingizi mzito, naye mtu mzembe huona njaa. 16Yeye ambaye hutii mafundisho huulinda uhai wake, bali yeye anayezidharau njia zake atakufa.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.