Mithali 15:27
Proverbs 15:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu, bali yeye achukiaye rushwa ataishi.
Proverbs 15:27 in English
Proverbs 15:27 · Berean Standard Bible
He who is greedy for unjust gain brings trouble on his household, but he who hates bribes will live.
Context
25Bwana hubomoa nyumba ya mtu mwenye kiburi,
bali huilinda mipaka ya mjane isiguswe. 26Bwana huchukia sana mawazo ya mwovu,
bali mawazo ya wale walio safi humfurahisha yeye. 27Mtu mwenye tamaa huletea jamaa yake taabu,
bali yeye achukiaye rushwa ataishi. 28Moyo wa mwenye haki hupima majibu yake,
bali kinywa cha mwovu hufoka ubaya. 29Bwana yuko mbali na waovu,
bali husikia maombi ya wenye haki.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.