Native Bible

Proverbs 15:19 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Njia ya mvivu imezibwa na miiba, bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu.

Proverbs 15:19 in English

Proverbs 15:19 · Berean Standard Bible

The way of the slacker is like a hedge of thorns, but the path of the upright is a highway.

Context

17Afadhali chakula cha mboga mahali palipo na upendo kuliko nyama ya ndama iliyonona pamoja na chuki. 18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi, bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi. 19Njia ya mvivu imezibwa na miiba, bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu. 20Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. 21Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili, bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.