Mithali 15:20
Proverbs 15:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, bali mtu mpumbavu humdharau mama yake.
Proverbs 15:20 in English
Proverbs 15:20 · Berean Standard Bible
A wise son brings joy to his father, but a foolish man despises his mother.
Context
18Mtu mwepesi wa hasira huchochea ugomvi,
bali mtu mvumilivu hutuliza ugomvi. 19Njia ya mvivu imezibwa na miiba,
bali njia ya mwenye haki ni barabara kuu. 20Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake,
bali mtu mpumbavu humdharau mama yake. 21Upumbavu humfurahisha mtu ambaye hana akili,
bali mtu mwenye ufahamu hushika njia iliyonyooka. 22Mipango hushindwa kufanikiwa kwa ajili ya kukosa ushauri,
bali kukiwa na washauri wengi hufanikiwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.