Native Bible

Proverbs 13:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri.

Proverbs 13:10 in English

Proverbs 13:10 · Berean Standard Bible

Arrogance leads only to strife, but wisdom is with the well-advised.

Context

8Utajiri wa mtu waweza kukomboa maisha yake, bali mtu maskini hasikii kitisho. 9Nuru ya mwenye haki hungʼaa sana, bali taa ya mwovu itazimwa. 10Kiburi huzalisha magomvi tu, bali hekima hupatikana kwa wale wanaozingatia ushauri. 11Fedha isiyo ya halali hupungua, bali yeye akusanyaye fedha kidogo kidogo huongezeka. 12Kilichotarajiwa kikikawia kuja moyo huugua, bali tumaini lililotimizwa ni mti wa uzima.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.