Mithali 12:9
Proverbs 12:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi, kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula.
Proverbs 12:9 in English
Proverbs 12:9 · Berean Standard Bible
Better to be lightly esteemed yet have a servant, than to be self-important but lack food.
Context
7Watu waovu huondolewa na kutoweka,
bali nyumba ya mwenye haki husimama imara. 8Mtu husifiwa kulingana na hekima yake,
bali watu wenye akili zilizopotoka hudharauliwa. 9Heri mtu wa hali ya chini mwenye mtumishi,
kuliko kujifanya mtu wa hali ya juu nawe huna chakula. 10Mtu mwenye haki hujali mahitaji ya mnyama wake,
bali matendo ya huruma ya mwovu ni ukatili. 11Yeye alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele,
bali yeye afuataye mambo ya upuzi hana akili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.