Mithali 12:16
Proverbs 12:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja, bali mtu wa busara hupuuza matukano.
Proverbs 12:16 in English
Proverbs 12:16 · Berean Standard Bible
A fool’s anger is known at once, but a prudent man overlooks an insult.
Context
14Kutokana na tunda la midomo yake
mtu hujazwa na mambo mema,
hakika kama ilivyo kazi ya mikono yake humtunza. 15Njia ya mpumbavu huonekana sawa
machoni pake mwenyewe,
bali mtu mwenye hekima husikiliza ushauri. 16Mpumbavu huonyesha kuudhika kwake mara moja,
bali mtu wa busara hupuuza matukano. 17Shahidi wa kweli hutoa ushuhuda wa kuaminika,
bali shahidi wa uongo husema uongo. 18Maneno ya kipumbavu huchoma kama upanga,
bali ulimi wa mwenye hekima huleta uponyaji.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.