Mithali 11:3
Proverbs 11:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Uadilifu wa wenye haki huwaongoza, bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao.
Proverbs 11:3 in English
Proverbs 11:3 · Berean Standard Bible
The integrity of the upright guides them, but the perversity of the faithless destroys them.
Context
1Bwana huchukia sana mizani za udanganyifu,
bali vipimo sahihi ni furaha yake. 2Kiburi kinapokuja, ndipo huja aibu,
bali unyenyekevu huja na hekima. 3Uadilifu wa wenye haki huwaongoza,
bali wasio waaminifu huharibiwa na hila yao. 4Utajiri haufaidi kitu katika siku ya ghadhabu,
bali haki huokoa kutoka mautini. 5Haki ya wasio na lawama, huwatengenezea njia iliyonyooka,
bali waovu huangushwa kwa uovu wao wenyewe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.