Native Bible

Proverbs 10:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu.

Proverbs 10:3 in English

Proverbs 10:3 · Berean Standard Bible

The LORD does not let the righteous go hungry, but He denies the craving of the wicked.

Context

1Mithali za Solomoni: Mwana mwenye hekima huleta furaha kwa baba yake, lakini mwana mpumbavu huleta huzuni kwa mama yake. 2Hazina zilizopatikana kwa njia mbaya hazifai, lakini uadilifu huokoa kutoka mautini. 3Bwana hawaachi waadilifu kukaa njaa, lakini hupinga tamaa ya mtu mwovu. 4Mikono mivivu hufanya mtu kuwa maskini lakini mikono yenye bidii huleta utajiri. 5Yeye akusanyaye mazao wakati wa kiangazi ni mwana mwenye hekima, lakini yeye alalaye wakati wa mavuno ni mwana mwenye kuaibisha.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.