Native Bible

Numbers 7:48 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake.

Numbers 7:48 in English

Numbers 7:48 · Berean Standard Bible

On the seventh day Elishama son of Ammihud, the leader of the Ephraimites, drew near.

Context

46mbuzi dume mmoja kwa ajili ya sadaka ya dhambi; 47maksai wawili, kondoo dume watano, mbuzi dume watano na wana-kondoo dume watano wa mwaka mmoja, ili vitolewe dhabihu kama sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deueli. 48Siku ya saba Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa watu wa Efraimu, alileta sadaka yake. 49Sadaka aliyoleta ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzito wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha la kunyunyizia lenye uzito wa shekeli sabini, vyote kulingana na shekeli ya mahali patakatifu, vikiwa vimejazwa unga laini uliochanganywa na mafuta kama sadaka ya nafaka; 50sinia moja la dhahabu lenye uzito wa shekeli kumi, likiwa limejazwa uvumba;

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.