Hesabu 25:12
Numbers 25:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye.
Numbers 25:12 in English
Numbers 25:12 · Berean Standard Bible
Declare, therefore, that I am granting him My covenant of peace.
Context
10Bwana akamwambia Mose, 11“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza. 12Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye. 13Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.” 14Jina la Mwisraeli ambaye aliuawa pamoja na mwanamke wa Kimidiani ni Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa jamaa ya Simeoni.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.