Hesabu 25:11
Numbers 25:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza.
Numbers 25:11 in English
Numbers 25:11 · Berean Standard Bible
“Phinehas son of Eleazar, the son of Aaron the priest, has turned My wrath away from the Israelites; for he was zealous for My sake among them, so that I did not consume the Israelites in My zeal.
Context
9Lakini wale waliokufa kwa hiyo tauni walikuwa watu 24,000. 10Bwana akamwambia Mose, 11“Finehasi mwana wa Eleazari, mwana wa kuhani Aroni, amegeuza hasira yangu mbali na Waisraeli, kwa sababu alikuwa na wivu kama nilio nao kwa heshima yangu miongoni mwao, hata kwamba kwa wivu wangu sikuwaangamiza. 12Kwa hiyo mwambie Finehasi ninafanya Agano langu la amani naye. 13Yeye pamoja na wazao wake watakuwa na Agano la ukuhani milele, kwa sababu alikuwa na wivu kwa ajili ya heshima ya Mungu wake, na akafanya upatanisho kwa Waisraeli.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.