Hesabu 24:8
Numbers 24:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Mungu alimleta kutoka Misri; yeye ana nguvu kama nyati. Anayararua mataifa yaliyo adui zake, na kuvunja mifupa yao vipande vipande; huwachoma kwa mishale yake.
Numbers 24:8 in English
Numbers 24:8 · Berean Standard Bible
God brought him out of Egypt with strength like a wild ox, to devour hostile nations and crush their bones, to pierce them with arrows.
Context
6“Kama mabonde, yanaenea,
kama bustani kando ya mto,
kama miti ya udi iliyopandwa na Bwana,
kama mierezi kando ya maji. 7Maji yatatiririka kutoka ndoo zake;
mbegu yake itakuwa na maji tele.
“Mfalme wake atakuwa mkuu kuliko Mfalme Agagi;
ufalme wake utatukuka. 8“Mungu alimleta kutoka Misri;
yeye ana nguvu kama nyati.
Anayararua mataifa yaliyo adui zake,
na kuvunja mifupa yao vipande vipande;
huwachoma kwa mishale yake. 9Hujikunyata na kuvizia kama simba,
kama simba jike; nani anayethubutu kumwamsha?
“Abarikiwe kila akubarikiye,
na alaaniwe kila akulaaniye!” 10Ndipo hasira ya Balaki ikawaka dhidi ya Balaamu. Akapiga mikono yake pamoja, akamwambia Balaamu, “Nilikuita uje kuwalaani adui zangu, lakini umewabariki mara hizi tatu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.