Native Bible

Numbers 23:24 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.”

Numbers 23:24 in English

Numbers 23:24 · Berean Standard Bible

Behold, the people rise like a lioness; they rouse themselves like a lion, not resting until they devour their prey and drink the blood of the slain.”

Context

22Mungu aliwatoa kutoka Misri; wao wana nguvu za nyati. 23Hakuna uchawi dhidi ya Yakobo, wala hakuna uaguzi dhidi ya Israeli. Sasa itasemwa kuhusu Yakobo na Israeli, ‘Tazama yale Mungu aliyotenda!’ 24Taifa lainuka kama simba jike; linajiinua kama simba ambaye hatulii mpaka amalize kurarua mawindo yake na kunywa damu ya mawindo yake.” 25Kisha Balaki akamwambia Balaamu, “Usiwalaani kabisa, wala usiwabariki kabisa!” 26Balaamu akajibu, “Je, sikukuambia ni lazima nifanye lolote analosema Bwana?”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.