Nahumu 3:14
Nahum 3:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, imarisha ulinzi wako, Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, yakanyage matope, karabati tanuru la kuchomea matofali!
Nahum 3:14 in English
Nahum 3:14 · Berean Standard Bible
Draw your water for the siege; strengthen your fortresses. Work the clay and tread the mortar; repair the brick kiln!
Context
12Ngome zako zote ni kama mitini
yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva;
wakati inapotikiswa,
tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. 13Tazama vikosi vyako:
wote ni wanawake!
Malango ya nchi yako
yamekuwa wazi kwa adui zako;
moto umeteketeza mapingo yake. 14Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako,
imarisha ulinzi wako,
Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi,
yakanyage matope,
karabati tanuru la kuchomea matofali! 15Huko moto utakuteketeza,
huko upanga utakuangusha chini
na kama vile panzi, watakumaliza.
Ongezeka kama panzi,
ongezeka kama nzige! 16Umeongeza idadi ya wafanyabiashara wako
mpaka wamekuwa wengi kuliko nyota za angani,
lakini kama nzige wanaacha nchi tupu
kisha huruka na kwenda zake.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.