Native Bible

Nahum 3:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Tazama vikosi vyako: wote ni wanawake! Malango ya nchi yako yamekuwa wazi kwa adui zako; moto umeteketeza mapingo yake.

Nahum 3:13 in English

Nahum 3:13 · Berean Standard Bible

Look at your troops— they are like your women! The gates of your land are wide open to your enemies; fire consumes their bars.

Context

11Wewe pia utalewa; utakwenda mafichoni na kutafuta kimbilio kutoka kwa adui. 12Ngome zako zote ni kama mitini yenye matunda yake ya kwanza yaliyoiva; wakati inapotikiswa, tini huanguka kwenye kinywa chake alaye. 13Tazama vikosi vyako: wote ni wanawake! Malango ya nchi yako yamekuwa wazi kwa adui zako; moto umeteketeza mapingo yake. 14Teka maji kwa ajili ya kuzingirwa kwako, imarisha ulinzi wako, Ufanyie udongo wa mfinyanzi kazi, yakanyage matope, karabati tanuru la kuchomea matofali! 15Huko moto utakuteketeza, huko upanga utakuangusha chini na kama vile panzi, watakumaliza. Ongezeka kama panzi, ongezeka kama nzige!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.